MWIGIZAJI raia wa Urusi, Polina Menshikh ameuawa katika tukio la mlipuko wakati akifanya onesho mbele ya vikosi vya jeshi nchini Ukraine. BBC imeripoti.
–
Tukio hilo limetokea November 19, imeelezwa Polina alialikwa kutoa burudani katika siku ya mapumziko ya vikosi vya jeshi la Ukraine.
–
Taarifa za vyombo vya habari nchini humo zinasema tukio hilo limetokea eneo la ukumbi wenye uwezo wa kubeba watu 150.
–
Shirika la Habari Uingereza (BBC) limesema limezungumza na msemaji wa jeshi la Ukraine kupitia idhaa ya BBC ya Ukraine, ambapo alithibitisha tukio hilo.


4 comments