Mwigulu aeleza umuhimu wa tozo

WABUNGE nchini waliamua kupitisha tozo mbalimbali, ili zisaidie miradi mikubwa ya kimkakati iliyopo nchini.

Kauli hiyo imetolewa muda mfupi uliopita mkoani Dodoma na Waziri wa Fedha na Mipango, Dk Mwigulu Nchemba, wakati akitoa ufafanuzi kuhusiana na masuala ya tozo.

Amesema wabunge waliamua kukubali kupitisha tozo hizo kwa sababu gharama mbalimbali za miradi ya kimkakati ikiwemo ujenzi wa Reli ya Kisasa, Ujenzi wa Bwawa la Umeme la Nyerere.

Pia amesema serikali inatoa elimu bure, huku ikitoa mikopo kwa wanafunzi na kusisitiza kuwa miradi ya kimkakati ina faida kuwa kwa Watanzania.

 

Habari Zifananazo

Back to top button