Mwigulu: “Pesa zimeibwa? Zimeenda wapi?”

DAR ES SALAAM: Waziri wa Fedha Dk Mwigulu Nchemba amehoji uhalali wa madai kuwa fedha zinaibwa huku maendeleo yakiendelea kupigwa katika nyanja ya afya.
Dk Mwigulu amesema kazi zinayofanywa na Serikiali chini ya Rais Samia Suluhu Hassan zinajiuza kutokana na dhamira na dira iliyowekwa.
Akizungumza katika hafla ya uzinduzi wa Ripoti ya Utafiti wa Afya ya Uzazi na Mtoto na viashiria vya Malaria Tanzania ya mwaka 2022 katika ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa Julius Nyerere (JNICC) Dar es Salaam leo, Oktoba 28, 2023, Waziri huyo amesema:
“Wengine wanaosema fedha zinaibiwa mimi swali langu limekuwa jepesi tu, kama fedha zinaweza zikaibiwa lakini bado ukatengeza vituo vya afya katika Tarafa zote tena vituo vya kisasa vinavyopatikana katika nchi zilizoendelea, ukanunua magari mengi, je wakati haziibiwi zilikuwa zinaenda wapi? kwasababu hivi ni vitu vinavyoonekana na vinanuliwa kwa fedha.”
Dk Mwigulu amesema Rais Samia amekuwa akitoa maelekezo ya fedha kutumika katika kutatua changamoto zinazoikumba jamii katika maeneo mbalimbali na matokeo yake yanaonekana.
3 comments

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *