Mwili mtoto wa miezi 5 waokotwa jalalani

MWILI wa mtoto mchanga anayekadiliwa kuwa na umri wa miezi mitano umekutwa umetupwa jalalani katika mtaa wa Shilabela Kata ya Buhalahala, mkoani Geita.

Ofisa wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Wilaya ya Geita, Edward Lukuba amethibitisha tukio hilo na kueleza taarifa hizo zilitolewa na raia mwema Machi 5, 2023 asubuhi.

Amesema mwili huo umekutwa tayari umeshaanza kuharibika, huku ukiwa umeshambuliwa na wanyama kwenye baadhi ya viungo kutokana na kuwa katika mazingira yasiyo salama.

“Tulipata taarifa hii kupitia simu yetu ya dharura 114, asikari wa zimamoto na uokoaji waliambatana na askari wa jeshi la polisi kitengo cha upelelezi, walikuta ule mwili umetupwa katika jalala.

“Walichukua ule mwili na kuupeleka katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa kwa taratibu zingine za kiupelelezi na hatukuweza kumpata aliyefanya kitendo hiki, lakini bado uchunguzi unaendelea, ili kuweza kumbaini.

“Tukio lililofanyika siyo la kibinadamu, kwa sababu unapokatisha uhai wa mtoto huwezi kujua pengine huyu mtu angekuja kuwa na mchango gani katika taifa letu la Tanzania na hata mkoa wetu wa Geita, ” amesema.

 

Habari Zifananazo

Back to top button