Mwili wa Josephine waagwa Lindi

LINDI: Mwili wa aliyekuwa Mwandishi wa habari wa Kampuni ya Sahara Media Group (Star tv) Mkoa wa Lindi, Josephine Kibiriti umeagwa leo mkoani Lindi.

Akizungumza wakati wa kuaga mwili huo, Paroko Msaidizi wa Parokia ya St. Francis Xavier Mkoa wa Lindi, Padre Pius Babu amewataka waumini wa dini zote kusali na kumuomba Mungu kwa bidii ili kuwa na mwisho mwema.

Josephine alifariki usiku wa Machi 25, 2024 kwa ajali ya gari iliyotokea maeneo ya Nyamwage mkoani Pwani akitokea Jijini Dar es salaam kuelekea mkoani Lindi.

Amesema wanapofanya matendo mema hapa Duniani yatawafanya wawe karibu na Mungu na kufuata misingi yake.

Mwili wa marehemu Josephine utasafirishwa kwenda wilayani Musoma Mkoa wa Mara kwa ajili ya mazishi.

Habari Zifananazo

Back to top button