Mwimbaji injili kushiriki Pasaka

MWIMBAJI wa nyimbo za Injili nchini Christopher Mwagila, amethibitisha kushiriki kwenye tamasha la Pasaka Aprili 9, mwaka huu Leaders Club jijini Dar es Salaam.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, Mwangila amesema watu wajitokeze kwa wingi katika Tamasha la Pasaka kufanyika Dar es Salaam.

“Tamasha la Pasaka nitakonga nyoyo za waumini mbalimbali wa nyimbo za injili na nitaimba live usipange kukosa lakini pia tujotokeze katika kumpongeza Rais Samia kwa kazi nzuri aliyoifanya ndani ya miaka miwili njoni tusifu kwa pamoja.” amesema Mwangila.

Advertisement

Kwa upande wake mwandaaji wa tamasha hilo Mkurugenzi wa Msama Promotioni, Alex Msama amesema nitamasha lisiloangalia dini wala dhehebu ya mtu yoyote anakaribisha hakuna kiingilio.

“Kila mtanzania anakaribidhwa kupongeza jitihada anazofanya mama kwakuwa alipokea nchi akiwa kwenye kipindi ligumu lakini bado tunafuraha upendo na amani katika taifa letu hivyo tamasha hili sio la kukosa njooni tumpongeze mama kwa pamoja.” amesema Msama

Katika tamasha hilo litaongozwa na waimbaji kama Upendo Nkone, Christopher Mwangira, Zabron Singer na wengine kutoka Kenya, Congo na Afrika kusini.

Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *