MAKAMU wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Hemed Suleiman Abdulla amesema Rais mstaafu wa awamu ya pili, Ali Hassan Mwinyi alipambana katika kuondoa rushwa, dawa za kulevya na mengine mabaya.
Kiongozi huyo amezungumza hayo leo katika hafla ya kutoa salamu za mwisho inayofanyika uwanja wa Amani Zanzibar.
Amesema misingi ya mafaniko katika taifa yanatokana na viongozi waliopita akiwemo Mwinyi na kwamba katika uhai wake alihimiza kushirikiana na serikali na sio kuiogopa.
“Hii kazi aliifanya kwa weledi mkubwa na sote tunaendelea kuindeleza katika awamu mbalimbali.
Lakin pia alikerwa sana na uzembe, uvivu ndani ya serikali.”