Mwinyimvua kidedea wazazi Arusha

MWENYEKITI wa Umoja wa Wazazi Mkoa wa Arusha, Ally Mwinyimvua, amemetetea nafasi yake ya uenyekiti kwa awamu ya pili na kumbwaga aliyekua Meya wa Jiji la Arusha, Gaudence Lyimo.

Uchaguzi huo ulifanyika jana ukumbi wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Arusha, ambapo kwa mujibu wa msimamizi wa uchaguzi huo, Anna Msuya, Mwinyimvua maarufu kwa kina la Meku alipata kura (212), huku Meya mstaafu Gaudence Lyimo akipata kura  61 na Bertha Laizer kura 1.

“Nasamehe yote yaliyotokea sasa hivi tujenge jumuiya yetu, yaliyopita si ndwele, nitaendelea kuwatumikia zaidi na zaidi, ” alisema Mwenyekiti huyo baada ya kuibuka mshindi.

Habari Zifananazo

Back to top button