Mzamiru bado yupo sana unyamani

DAR ES SALAAM: KLABU ya Simba imefanikiwa kumbakiza kiungo wao Mzamiru Yassin kwa mkataba wa miaka miwili.

Mzamiru ni mchezaji wa tatu kuongeza mkataba ndani ya timu hiyo kwa  hivi karibuni akiwemo mshambuliaji wao Kibu Denis na Israel Mwenda. Wote mikataba yao imemalizika msimu huu.

Imeelezwa kuwa Simba wamefanikiwa kumpa Mzamiru mkataba wa miaka miwili baada ya mazungumzo kwenda vizuri na kusalia ndani ya kikosi cha wekundu wa Msimbazi.

“Ni kweli Mzamiru mkataba wake upo ukingoni na ameshamalizana na mabosi kwa kusaini mkataba mwingine wa miaka miwili. Mazungumzo na wachezaji wengine yanaendelea akiwemo Kipa Ayoub Lakred na yapo katika hatua nzuri,” kimesema chanzo hicho.

SOMA: Hatma ya Simba, mikononi mwa Geita Gold FC

Meneja wa Idara ya Habari na Mawasiliano wa Simba, Ahmed Ally amekiri kuna baadhi ya wachezaji wataongeza mkataba ambayo inafikia ukingoni na baadhi yao wakiwa katika hatua nzuri ya mazungumzo.

Amesema kuna wachezaji ambao wapo kwenye mipango ya timu wataongezewa mkataba kwa ambaye inamalizika msimu huu na kuongeza mpya ambapo wamependekezwa na benchi la ufundi kulingana na mahitaji yao.

“Msimu huu hatukufanya vizuri kwenye ligi, hatujatimiza malengo yetu ikiwemo Ubingwa wa Ligi na Kombe la Shirikisho (FA) kuondolewa robo fainali. Tumeona sababu ya kutofikia huko na tunaenda kuboresha timu.

Maboresho makubwa yanakuja ndani ya Simba kwa msimu ujao kwa kusajili wachezaji wazuri na wenye viwango bora kusaidia kufikia malengo kwa msimu ujao wa mashindano,” amesema Ahmed na ameongeza kuwa:

Mwekezaji wetu Mohammed Dewji ameamua kuongeza mguvu kwenye usajili na kuweka kiasi kikubwa cha fedha, kupata wachezaji wenye ubora na kuirudisha Simba bora na imara kwa msimu ujao.

Simba msimu huu hawakufanya vizuri na kushundwa kuomyesha upinzani mbele ya watani wao wa jadi, Yanga kwa kukubali kupoteza mechi zote mbili na  waliondolewa kombe la Shirikisho la CRBD Bank hatua ya robo fainali na Mashujaa FC uwanja wa Lake Tanganyika, Kigoma.

Wekundu hao wa Msimbazi wamefanikiwa kutwaa kombe la Ngao ya Jamii kwa kumfunga Yanga kwa ushindi wa penalti wa mabao 3-1  na kombe la Muungano visiwani Zanzibar kwa kumfunga Azam FC  1-0.

Habari Zifananazo

Back to top button