Rais Mstaafu wa awamu ya pili wa Tanzania, Ali Hassan Mwinyi amefariki Dunia leo Februari 29, 2024 majira ya saa 11:30 jioni katika Hospitali ya Mzena, Jijini Dar es Salaam alipokuwa akipatiwa matibabu ya ugonjwa wa saratani ya mapafu.
Rais Samia Suluhu Hassan ametangaza kifo cha kiongozi huyo aliyewahi kuwa Makamu wa Rais, Rais Zanzibar na Rais wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kipindi cha miaka 10, kuanzia mwaka 1985 hadi 1995.
View this post on Instagram
Mzee Mwinyi amekuwa akipatiwa matibabu tangu November 2023 London Uingereza na baadaye kurejea nchini na kuendelea na matibabu Jijini Dar es Salaam.
Rais Samia ametangaza siku saba za maombolezo kuanzia kesho Machi 1. Mzee Mwinyi atazikwa Unguja, Machi 2, 2024.