Mzee Mwinyi augua kifua, alazwa

DAR ES SALAAMl Rais Mstaafu wa Awamu ya Pili wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mzee Ali Hassan Mwinyi amepelekwa hospitali akiugua maradhi ya kifua.

Taarifa kutoka kwa mtoto wa mzee Mwinyi ambaye ni msemaji wa familia, Abdullah Ali Mwinyi amesema, Mzee Mwinyi anaendelea kupata matibabu chini ya uangalizi wa karibu wa madaktari.

“Kutokana na ushauri wa madaktari wake, familia imeona ni vyema apate faragha akiwa anapatiwa matibabu. Hivyo Familia inaiomba jamii kumkumbuka kwenye Dua, Sala, na Maombi,” amesema Abdullah

Advertisement

Aidha, amesema wanamuomba  Mwenyezi Mungu amjaalie shifaa ya haraka Mzee wao pamoja na wagonjwa wengine wote wanaokabiliwa na maradhi mbali mbali.