DAR ES SALAAM: BAADHI ya wachezaji wa Yanga waliokuwa kwenye kambi ya timu ya taifa ‘Taifa Stars’ wamerejea nchini kujiandaa na mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika.
Taarifa iliyotolewa leo na ofisa habari wa klabu hiyo, Ali Kamwe amewataja wachezaji hao kuwa ni Clement Mzize, Mudathir Yahya na Ibrahim Bacca.
“TFF wameruhusu baadhi ya wachezaji wetu ambao walikuwa kwenye kambi ya timu ya taifa kurejea mapema kwa ajili ya kuanza maandalizi kuelekea mchezo wa Mamelodi,” Ali Kamwe.
Machi 30, Yanga itawakaribisha Mamelodi Sundowns katika mchezo wa robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika (CAFCL) utakaopigwa kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa Dar es Salaam.