Mzize: Ubingwa una maana kubwa kwangu

MSHAMBULIAJI chipukizi wa Yanga, Clement Mzize amesema ubingwa waliochukua jana unamaana kubwa katika historia ya maisha yake ya soka la ushindani.

Akizungumza na HabariLEO, mshambuliaji huyo amesema mafanikio hayo yatamuongezea ari ya kuzidi kujituma ili aweze kufanya vizuri zaidi siku zijazo akiwa na miamba hiyo ya Tanzania Bara.

“Namshukuru Kocha wangu Nasreddine Nabi kwangu ni kama baba kutokana na ushauri anaonipa lakini pia ni mtu mwenye imani kubwa na mimi hilo linanifanya kuongeza bidii na kujituma ili nimfurahishe,” amesema Mzize.

Mshambuliaji huyo amesema kwa nafasi aliyopewa ataendelea kupambana ili msimu unaokuja aweze kufanya vizuri zaidi ikiwemo kuwa tegemezi kwenye kikosi cha kwanza.

Habari Zifananazo

Back to top button