CHUO Kikuu Mzumbe kwa kushirikiana na Shirika la Kuhudumia Viwanda Vidogo (Sido) wametoa mikopo kwa njia ya mtandao (C4YET) kutoka Shirika la Kimataifa la Maendeleo Denmark (DANIDA) kwa wajasiriamali zaidi ya 100.
Akizungumza na wanahabari jijini Arusha kuhusu mradi huo,Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Mzumbe,Profesa William Mwegoha amesema mradi huo umewezesha vijana kuanisha aina ya biashara wanaofanya sanjari urejeshwaji wa mikopo yenye riba ya chini kulingana na mkopo waliyopewa kutokana na biashara wanaofanya.
Chuo hicho kiliona changamoto wanazopata wajasiriamali wadogo ambapo hawawezi kukopesheka kwa urahisi na ndio ikatumia njia ya kufanya tafiti juu ya changamoto za ajira na hatimaye kuchagiza sekta ya ajira ili vijana wa kitanzania kuchangia shughuli za kiuchumi sanjari na kunufaika na ajira kupitia mradi huo.
“Mradi huu ulianza mwaka 2019 na mwakani unatarajia kuisha lakini mafanikio ni makubwa kwa vijana kuweza kukopesheka ikiwemo kujikwamua kiuchumi kupitia Sido ”
Naye Mratibu wa mradi huo,Dk,Nsubili Isaga kutoka skuli ya biashara chuo Kikuu Mzumbe akielezea kuhusu mradi huo amesema vijana wengi hawakubaliki kukopesheka benki kutokana ukosefu wa mali zisizohamishika hivyo watafiti hao kutoka Mzumbe waliamua kutafuta njia ya kuwezesha vijana kujiajiri ikiwemo ongezeko la ajira.
Amepongeza kuwa mradi huo awali ulianza kukaa na wanataaluma lakini badae ukaenda kwa wajasiriamali kutokana na kubuni nyenzo walizotum za uandishi wa andiko liliwavuta wafadhili kwaajili ya washirika kusaidia tafiti na hatimaye chuo hicho kushirikisha Sido kwaajili ya kuwakwamua wajasiriamali vijana kwenye mikoa mitano ambayo ni Arusha,Mwanza,Dar es Salama , Morogoro na Mbeya.
Huku wajasiriamali 187 walipewa mafunzo hayo ambapo wajasiriamali 100 kati yao waliweza kupata mikopo yenye riba ya asilimia 5 tu inayowawezesha wao kurejesha mikopo yao kwa wakati na badae vijana wengine watafikiwa zaidi ili wajiunge na majukwaa ya biashara mitandaoni.