Mzumbe watakiwa kuharakisha jambo lao Tanga

Mzumbe watakiwa kuharakisha jambo lao Tanga

UONGOZI wa Chuo Kikuu cha Mzumbe, umetakiwa kuharakisha utekelezaji wa mradi wa ujenzi wa kampasi ya chuo hicho katika Wilaya ya Mkinga, mkoani Tanga.

Msisitizo huo umetolewa na Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Waziri Kindamba alipotembelewa na uongozi wa chuo hicho ofisini kwake leo.

” Ni muhimu ujenzi  wa kampasi hiyo ya Mzumbe uanze mapema,  kwani tayari eneo lishapatikana na wanatanga wanahitaji uwepo wa chuo hicho kwa ajili ya maendeleo yao,”amesema RC Kindamba.

Advertisement

Amesema ofisi yake itaendelea kutoa ushirikiano wa karibu kwa chuo hicho katika kuhakikisha malengo ya mradi huo yanafikiwa na kuwanufaisha wananchi wa Tanga.

Naye Kaimu Makamu Mkuu wa chuo Prof. William Mwegoha, amesema tayari chuo kimekamilisha mpango wa matumizi bora ya ardhi eneo lililotengwa kwa ajili ya ujenzi.

“Baada ya tathimini hiyo tutangaza zabuni, ili kumpata mkandarasi atakayehusika kufanya tathmini ya athari za kijamii na mazingira, ili ujenzi uanze,”amesema Mwegoha.