Mzungu aachana na Simba

MCHEZAJI Mzungu wa Simba, Dejan Georgijevic jana alitangaza rasmi kuvunja mkataba na klabu hiyo.

Hata hivyo, pamoja na taarifa hizo kuzagaa katika mitandao ya kijamii, lakini uongozi wa klabu hiyo ulikana

taarifa ya kuachana na mshambuliaji huyo raia wa Serbia.

Dejan tayari ameondoka kambini visiwani Zanzibar na kurejea Dar es Salaam kwa ajili ya kukamilisha baadhi ya taratibu, baada ya kuhudumu ndani ya timu hiyo kwa miezi miwili tangu alipojiunga nao akitokea klabu ya Domzare inayoshiriki Ligi Kuu ya Slovenia.

Hadi anavunja mkataba wake na Simba, Dejan amecheza jumla ya michezo sita ya mashindano tofauti, huku akiwa amefunga bao moja akiwa amecheza jumla ya dakika 312.

Akizungumza na HabariLEO jana, Mwenyekiti wa Simba, Murtaza Mangungu, alisema kuwa hawana taarifa ya kuvunjwa mkataba huo, Simba ni timu kubwa ina wachezaji wengi, hivyo haiwezi kulitolea ufafanuzi suala ambalo halijafika mezani kwao.

“Jambo hili linatupa wakati mgumu kulitolea ufafanuzi, yeye ametoa taarifa yake kwenye mitandao ya kijamii, sisi hatuwezi kuijibu kila taarifa inayoandikwa na mchezaji kwenye mtandao wa kijamii kama litafika mezani tutalitolea ufafanuzi,” alisema Mangungu.

Mshambuliaji huyo alitumia mtandao wa kijamii wa Instagram kuwaaga waajiri wake pamoja na mashabiki waliokuwa wakimpa sapoti tangu alipotua mitaa ya Msimbazi.

“Ninathibitisha kwamba mkataba wangu wa ajira umesitishwa kwa sababu za ukiukwaji wa kimsingi wa mkataba na klabu.”

“Asanteni mashabiki kwa sapoti na upendo mlionipa,” aliandika Dejan kwenye mtandao wake wa kijamii wa Instagram.

Dejan ameondoka Simba ikiwa ni siku kadhaa zimepita tangu waingie kwenye mgogoro na kiungo Augustine Okrah, baada ya mchezo wao wa kirafiki na Malindi ambao waliibuka na ushindi wa bao 1-0.

Habari Zifananazo

Subscribe
Notify of
guest
0 Comments
Inline Feedbacks
View all comments
Back to top button
0
Would love your thoughts, please comment.x
()
x