Nabi akili nyingi mechi na Watunisia

KOCHA wa Yanga, Nasreedin Nabi amekataa kuwataja wachezaji wawili watakaosekana kwenye mchezo wa kesho wa Kombe la Shirikisho Barani Afrika dhidi ya Club Africain ambao waliumia kwenye mchezo wa Ligi Kuu NBC dhidi ya Geita Gold wikiendi iliyopita.

Nabi amesema anafahamu uzito wa mchezo huo, hivyo kuwataja wachezaji hao ni kuwapa wapinzani wao nafasi ya kutumia udhaifu kwenye maeneo wanayocheza wachezaji hao.

Kocha huyo ametaja ubora wa wapinzani wao katika maeneo tofauti na kuongeza kuwa kubwa zaidi watacheza kwa tahadhari ili kutoruhusu goli.

“Club Africain wana timu nzuri na wachezaji wenye uzoefu pamoja na wachezaji chipukizi. Ni wazuri kwenye mipira ya kufa na mashambulizi ya haraka, pamoja na kwamba tunahitaji matokeo mazuri nyumbani pia tutacheza kwa tahadhari tusiruhusu goli,” amesema Nabi.

Yanga watacheza mchezo wa kwanza wa Kombe la Shirikisho kwenye Uwanja wa Mkapa, Dar es Salaam kesho, kabla ya kurudiana na wapinzania wao wiki moja baadaye.

 

 

 

Habari Zifananazo

Back to top button