Nabi awafariji Yanga matokeo na Simba

BAADA ya kipigo cha mabao 2-0 kutoka kwa watani zao Simba, Kocha Mkuu wa Yanga Nasreddine Nabi, amesema pamoja na timu yake kupoteza mchezo huo, lakini lazima watatetea ubigwa wao wa Ligi Kuu Tanzania Bara msimu huu.

Akizungumza na HabariLEO, kocha huyo ameeleza kuwa mikakati yao kwa sasa ni kuweka nguvu,  ili kuhakikisha wanashinda mechi zao nne zilizobaki, ili kubeba taji hilo.

“Tumekubali matokeo,  lakini kufungwa na Simba tumepoteza pointi tatu siyo ubingwa, bado Yanga tunayo nafasi ya kutetea taji letu,  kwa sasa tunajipanga ili kuweka mikakati ya kupata ushindi kwenye mechi nne zilizobaki,” amesema.

Yanga iliyopo kileleni mwa msimamo wa ligi na pointi 68, inahitaji kushinda mechi tatu kati ya nne zilizobaki ili kufikisha pointi 77 ambazo hazitoweza kufikiwa na Simba iliyopo nafasi ya pili na pointi 63 hata kama itashinda mechi zote nne zilizobaki.

Habari Zifananazo

Back to top button