KOCHA wa Yanga, Nasreddine Nabi amesema atazitumia siku chache zilizobaki kutengeneza mpango maalumu utakao wapa ushindi katika mchezo wa kwanza wa Fainali wa Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya USM Algers ya Algeria.
Akizungumza na HabariLEO, wakati timu hiyo ikirejea Dar es Salaam kutoka Singida ambako jana ilicheza mechi ya Nusu Faianili wa Kombe la Shirikisho la Azam (ASFC) dhidi ya Singida Big Stars, kocha huyo amesema anajua pakuwashika wapinzani wao na hiyo inatokana na kujua mbinu zao na ubora waliokuwa nao.
“Tuna dakika 180 za damu na jasho kwakua tunaanza nyumbani lazima tuzitumie dakika 90 za nyumbani kumaliza mchezo, nawajua vizuri wapinzani ikiwemo mbinu watakazo tumiwa wakiwa hapa lakini nitazitumia vizuri siku zilizobaki ili kuwamaliza kama ilivyokuwa kwa Marumo Gallants,” amesema Nabi.
Yanga itacheza mechi ya kwanza dhidi ya USM Algers Mei 28 uwanja wa Benjamin Mkapa kabla timu hizo kurudiana Juni 03 nchini Algeria.
Comments are closed.