NACTE yatoa ufafanuzi wanaopotelewa vyeti

BARAZA la Mitihani Tanzania (NACTE) limewataka watanzania wanaopotelewa na vyeti vya shule kutumia tovuti yao www.necta.go.tz na ndani ya mwezi mmoja mhusika atapigiwa simu.

Akizungumza jana Jijini Arusha katika Maonyesho ya Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi Stadi (NACTVET),Ofisa Habari na Uhusiano wa NACTE amesema endapo mtu amepoteza cheti aende Polisi kutoa taarifa (lose report)kisha atangaze kupitia magazeti na baada ya tangazo kutoka mhusika ajaze taarifa zake kupitia tovuti hiyo badala ya kupanda gari kwenda ofisi za baraza Dar es Salaam.

Amesema tangazo hilo linapaswa kuwana jina la mhusika,namba yake ya mtihani,shule aliyosoma na picha zitumwe ikiwemo mwaka uliomaliza kusoma.

“Nenda kwenye tovuti ya baraza la mitihani la wwww. nectar.go.tz na utaambatanisha taarifa ya polisi,tangazo lililotoka katika gazeti na picha za mhusika lakini pia unatakiwa uwe nankutambulishi cha mpigakura,leseni ya gari au hati ya kusafiria kama kitambulisho Taifa au cha mpigakura ”

Alisisitiza sio lazima tangazo la upotevu wa cheti likitoka uende ofisi za Nacte bali unatumia tovuti hiyo kwaaajili ya kuingiza taarifa zako kisha baada ya mwezi mmoja utapigiwa simu kuulizwa cheti chako kitumwe kwanjia gani.

Habari Zifananazo

Back to top button