Nahodha Geita awapa heshima Simba

NAODHA wa kikosi cha wachimba dhahabu wa Geita Fc Elias Maguli amefunguka na kusema kuwa kuelekea katika mchezo wao wa kesho dhidi ya Simba SC utakaopigwa kwenye dimba la CCM Kirumba Mwanza hautakua mchezo rahisi kwani wanatambua Simba ni timu kubwa na ina wachezaji wazuri.

Akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari kuelekea mchezo katika mchezo huo Maguli amesema kuwa kama wachezaji wanafanahamu ubora wa simba lakini wamejianda kupata matokeo mazuri  ikizingatiwa wapo katika uwanja wa nyumbani.

“Sisi kama wachezaji tumejiandaa vizuri kuelekea mchezo wa kesho tunajua Simba ni timu ya aina gani ina Wachezaji wazuri tunajua wamejiandaa vizuri kuja kupambana na sisi lakini tumejiandaa vizuri kuhakikisha tunapata matokeo ukizingatia tupo katika uwanja wa nyumbani”….Alisema

Hadi sasa kikosi cha Geita Gold fc kimecheza michezo 13 ikifanikiwa kukusanya pointi 16 huku kikiiwa nafasi ya 10 katika msimamo wa ligi kuu.

Habari Zifananazo

Back to top button