NAHODHA wa kata ya Kayenze Moro Masalu Kakolanya ameahidi timu yao itapambana kushinda michezo yao miwili iliyobakia katika kundi D kwenye mashindano ya The Angeline Jimbo cup, inayoendelea jijini Mwanza.
Masalu ametoa ahadi hiyo mara baada ya mchezo dhidi ya Sangabuye ulioisha kwa sare ya bao 1-1 katika uwanja wa shule ya msingi Bugogwa.
Bao la Kayenze lilifungwa na Kulwa Secko katika dakika ya 26 na Sangabuye walisawazisha kwa Florent Godwin katika dakika ya 55.
Masalu amesema timu yao imebakiza mechi dhidi ya Bugogwa na Shibula.
Katika mchezo wa kundi A uliochezwa kwenye uwanja wa Kona ya Bwiru, Nyamanoro ilitoka sare ya bao 1-1 dhidi ya Pasiansi.
Katika mchezo wa kundi B, Kahama ilishinda kwa mabao 2-1 dhidi ya Nyamhongolo katika mchezo uliochezwa uwanja wa shule ya sekondari Buswelu.
Tembelea //epaper.tsn.go.tz kusoma zaidi.
–
una maoni usisite kutuandikia
Comments are closed.