Naibu CAG Zanzibar aapishwa

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk Hussein Mwinyi amemuapisha Dk Said Khamis Juma kuwa Naibu Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.

Hafla hiyo ya uapisho imefanyika Ikulu Zanzibar kabla ya kuanza kikao cha Tume ya Mipango.

Rais Dk Mwinyi ameendelea kuweka msisitizo katika kuimarisha utawala bora, uwazi, na uwajibikaji katika Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, lengo likiwa ni kuhakikisha ufanisi wa matumizi ya rasilimali za umma.

Dk Said Khamis Juma Naibu Mdhibiti na Mkaguzi wa Hesabu za Serikali atamsaidia Dk Othman Abbas Ali Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali Zanzibar kuhakikisha matumizi ya fedha za umma yanafanyika kwa uwazi, ufanisi, na kwa mujibu wa taratibu na kanuni zilizopo.

Habari Zifananazo

Subscribe
Notify of
guest
0 Comments
Inline Feedbacks
View all comments
Back to top button
0
Would love your thoughts, please comment.x
()
x