NAIBU Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi na Mbunge wa Butiama, Jumanne Sagini, ameishukuru serikali ya a ya Rais Dk Samia Suluhu Hassan ndani ya kipindi cha miaka miwili ya uongozi wake, Chuo Kikuu cha Mwalimu Nyerere cha Kilimo na Teknolojia (MJNUAT) cha Butiama kina kwenda kufunguliwa na kuanza kuchukua wanafunzi Novemba mwaka huu (2023).
Sagini alisema hayo Juni 9, 2023 baada ya kushuhudia utiaji saini wa Hati ya mikataba miwili ushirikiano baina ya Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo (SUA) na Chuo Kikuu cha Mwalimu Nyerere cha Kilimo na Teknolojia (MJNUAT) cha Butiama kwenye halfa iliyofanyika Kampasi kuu ya Edward Moringe mkoani Morogoro.
Katika utioaji wa hati ya ushirikiano huo , mgeni rasmi alikuwa ni Katibu mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Profesa Carolyne Nombo kwa niaba ya Waziri wake .
“ Licha ya juhudi za wizara yetu kuania Katibu mkuu na Waziri kusimamia hili hadi kufikia hatua hii , shukrani zangu za kipekee ni kwa Rais Dk Samia Suluhu Hassan ameingia madarakani Machi 19, 2021 lakini ndani ya miaka miwili michakato imekamilika , maamuzi yamefanyika Chuo kinaenda kuanza …” alisema Sagini
“ Ni tangu mwaka 2012 licha ya dhamira nzuri ya marais waliomtagulia lakini imechukua muda mrefu bila kuanza mafunzo “ alisema Sagini ambaye ni Naibu Waziri na Mbunge wa Butiama
Sagini alimshukuru Rais Dk Samia kwa kuidhinisha fedha nyingi bilioni 102 zianzishe Chuo Kikuu na kwa kupitia wasaidizi wake Waziri Profesa Mkenda imetoa Sh bilioni 2.6 kuanza ukarabati wa majengo yaliyopo na kuridhia fedha hiyo ili ukaratabi uanze na kuwezesha Novemba 2023 wanafunzi kuanza masomo na pia kuifanya Butiama kupata hadhi tofauti na awali.
“ Hivyo nikiwa Mbunge wa Butiama na wananchi wite wa mkoa wa Mara , tunaishukuru Serikali , wizara na Vyuo Vikuu hivi viwili hususani SUA kwa kukubali kushrikiana na Chuo cha MJNUAT” alisema Sagini