Naibu Waziri asifu watoto umahiri mashindano baiskeli

NAIBU Waziri wa Habari, Sanaa na Utamaduni, Hamisi Mwijuma amewasifu watoto watatu wa familia moja baada ya kuonyesha umahiri wao wa kuendesha baiskeli zaidi ya kilomita 5 kwenye mbio za Swahili Marathon msimu wa kwanza zilizofayika jijini Arusha.

Watoto hao ni Andy Mlay (12), Alton Mlay(5), Joshua Mlay (5) pamoja na mama yao mzazi Naomi Kimaro.

Naibu Waziri huyo maarufu kama ‘MwanaFA‘ amewasifu na kutoa zawadi kisha kutoa ombi kwa watoto wengine kujitokeza kuendesha baiskeli na michezo mingine ili kukuza vipaji.

“Nawaona watoto hawa namlinganisha na mwanangu ninakuwa na hofu akiendesha baiskeli mwenyewe lakini kumbe watoto wanaweza heko sana watoto hawa mmeonyesha vipaji na wazazi wengine muibue vipaji vya watoto wenu”

‘Mwana FA’ ametoa rai hiyo wakati wa ufunguzi wa mbio za masafa za Swahili Marathon -msimu wa kwanza kwenye viwanja vya Nanenane Njiro, Jijini Arusha na kuongeza kuwa lugha ya Kiswahili lazima ipewe hadhi yake.

Habari Zifananazo

1 Comment
Oldest
Newest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments
Back to top button