Naibu Waziri awapongeza gofu Lugalo

NAIBU Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Hamisi Mwinjuma ameipongeza Klabu ya Gofu ya Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) Lugalo kwa kuendeleza uhusiano mwema wa jeshi na raia.

Akizungumza katika sherehe za ufungaji wa mashindano ya NBC Lugalo Open 2023, zilizofanyika jijini Dar es Salaam, Naibu Waziri huyo amesema, Lugalo Gofu imekuwa ikishirikiana vizuri na raia.

“Niwapongeze kwa kushirikiana vizuri katika shughuli mbalimbali za kijamii hasa za kimichezo tofauti na maeneo mengi ya jeshi hapa nchni tulivyozoea,” amesema.

Naye Mwenyekiti wa Klabu ya JWTZ Lugalo, Brigedia Jenerali Mstaafu Michael Luwongo, ameishukuru Benki ya NBC kwa kudhamini mashindano hayo pamoja na kuundelea kukuza mchezo wa gofu nchini.

Kwa upande wa watoto Omari Shabani wa Lugalo, ameshika nafasi ya kwanza akifuatiwa na Julias James, huku wanawake mshindi ni Hawa Wanyeche wa Lugalo Gofu akifiatiwa na Vicky Elias wa Lugalo kwa mikwaju 162.

Upande wa wanaume Division C nafasi ya kwanza ikishikiliwa na Boniface Japhet wa Lugalo, huku Division B Nsajigwa Mwansasu wa Lugalo aliibuka kidedea, akifatiwa na Sigi Urassa. Division A nafasi ya kwanza imekamatwa na Samuel Kileo wa Lugalo, akifatiwa na Claud Mtavangu.

Mshindi wa Jumla wa mashindano hayo ni Ali Isanzu wa TPC Moshi aliyepiga, akifuatiwa na Michael Massawe wa Lugalo

Habari Zifananazo

Back to top button