Naibu Waziri Masanja akabidhi vifaa vya mazoezi kwa wenye uhitaji

Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mary Masanja amekabidhi vifaa mbalimbali vya mazoezi ya viungo kwa watoto wenye ulemavu wanaoishi pembezoni mwa Pori la Akiba la Pande ikiwa ni sehemu ya tamasha la kuhamasisha utalii wa ndani.

Tamasha hilo limefanyika Novemba 19,2022 lilihusisha utalii wa michezo ya mbio za baiskeli na mbio za kukimbia kwa miguu katika Pori la Akiba la Pande jijini Dar es Salaam.

“Washiriki wote waliokimbia mbio za baiskeli kilomita 33, Mbio za kukimbia kwa miguu kilomita 21,10, na 5 kiingilio kilichotoka kimeweza kuchangia upatikanaji wa vifaa vya hawa watoto wenye ulemavu” Masanja amesisitiza

Aidha,amewahamasisha watanzania wengine wenye uzalendo kuendelea kujitokeza kuchangia kundi hilo la watoto wenye ulemavu.

Amesema matamasha kama hayo yataendelea kufanyika katika maeneo mengine ya hifadhi ili kuunga mkono juhudi za Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan za kutangaza vivutio vya utalii nchini na kufungua fursa za uwekezaji.

Tamasha hilo lilihusisha washiriki kutoka maeneo mbalimbali nchini kutoka katika Taasisi za Serikali na Zisizo za Kiselikali.

Habari Zifananazo

Subscribe
Notify of
guest
0 Comments
Inline Feedbacks
View all comments
Back to top button
0
Would love your thoughts, please comment.x
()
x