Naibu Waziri Ndejembi atembelea Banda la NEC

Naibu Waziri, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Deogratius Ndejembi, leo Jumapili Agosti 6, 2023 ametembelea Banda la Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) katika viwanja vya Nzuguni yanapofanyika maonesho ya Nanenane Kanda ya Kati.

Akiwa katika banda hilo alipokea maelezo kutoka kwa Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Habari na Elimu ya Mpiga Kura (Elimu), Monica Mnanka namna uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura linavyofanyika .

Habari Zifananazo

Back to top button