NAMIBIA wameibuka mabingwa katika mashindano ya kriketi ya kufuzu Kombe la dunia kwa nchi za Afrika kwa wanaume chini ya miaka 19.
Ubingwa huo umepatikana baada ya timu hiyo kuitoa Kenya.
Akizungumza siku ya jijini Dar es Salaam jana, Julai 30, 2023 Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo, Pindi Chana wakati wakifunga mashindano hayo aliwapongeza Namibia kwa ushindi na kuwashukuru waandaaji kwa kuichagua Tanzania kuwa mwenyeji wa mashindano hayo,
“Nchi yetu inashiriki mashindano mbalimbali ndani na nje ya nchi, tuna program mbalimbali za vijana, tunandelea kukarabati na kujenga miundombinu mipya ya michezo, tunaamini kuwepo kwenu hapa nchini mmefurahia utamaduni wetu na mtarudi tena.” alisema Pindi.
Mashindano hayo yalijumuisha wanamichezo 84, na wataalam 25 kutoka nchi za Nigeria, Siera Lione, Uganda, Kenya, Namibia na wenyeji Tanzania.