Namungo na Kitambi ndio basi tena

LINDI: Klabu ya Namungo imetangaza kuachana na kocha ,Denis Kitambi kuanzia leo Desemba 13, 2023.
Taarifa iliyochapishwa kwenye kurasa rasmi za mitandao ya klabu hiyo imeeleza kuwa klabu inaheshimu mchango wa kocha huyo kwa kipindi chote alichohudumu ndani ya timu hiyo.
”Namungo Fc inamtakia kila la kheri Kocha, Denis Kitambi katika safari yake ya ukocha nje ya Namungo Fc imeongeza taarifa hiyo.
Ikumbukwe Kitambi alikuwa kocha msaidizi wa Namungo katika kipindi cha kocha, Cedric Kaze na Kaze alipoondoka kocha huyo alirithi mikoba yake.
Ameiacha timu hiyo katika nafasi ya sita kwenye msimamo wa Ligi Kuu Tanzania Bara ikiwa na alama 17 baada ya michezo 13.

Habari Zifananazo

Back to top button