Nandy ajifungua mtoto wa kike

Nandy: Mashabiki msiulizie masuala ya familia yangu

Msanii huyo ambaye ni mke wa msanii mwingine mahiri nchini William Lyimo ‘Billnass’, ameandika katika ukurasa wake wa instagram akishukuru kujifungua.

“Kwanza kabisa nimshukuru Mungu kwa ukuu wake hakika amezaliwa binti wa kichaga.. nikisema niongee yote sitomaliza leo ila nachoweza kusema nakupenda sana mama maana nimeona umuhimu na ugumu wa kukamilisha kuitwa mama.

‘Nyie na furaha sijawahi kupata maishani mwangu nilijua nimefurahi na mengi lakini kumbe bado,,,!!! hii ni furaha ya kweli toka moyoni,”ameandika Nandy na kumshukuru pia mumewe kwa mtoto huyo.

Advertisement