UNGUJA, Zanzibar: MWENYEKITI wa Chama cha Mapinduzi (CCM) na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, akiongoza Kikao Maalum cha Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya CCM kinachofanyika leo Januari 15, 2023 Unguja, Zanzibar.
Pamoja na masuala mengine, macho na masikio ya wanachama wa CCM ni kwa Katibu Mkuu mpya ambaye atarithi mikoba ya Daniel Chongolo aliyebwaga manyanga kwa kujiuzulu wadhifa huo hivi karibuni.
Chongolo alijiuzulu kwa kile alichodai ni kuchafuliwa kwenye mitandao ya kijamii.
Tangu kujiuzulu kwa Chongolo, wanachama na mashabiki wa chama hicho wamekua wakipigia ramli makada mbalimbali warithi wa Chongolo.