Nanyamba wapatiwa gari ya wagonjwa
HOSPITALI ya Halmashuri ya Mji wa Nanyamba mkoani Mtwara imekabidhiwa gari litalosaidia kubebea wagonjwa lenye thamani ya Sh milioni 240.
Akizungumza wakati wa zoezi la kukabidhi gari hilo, Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo, Jamal Kapende amesema kila mmoja kwa nafasi yake ikiwemo watendaji na wananchi katika halmashauri hiyo wana wajibu wa kuhakikisha gari hiyo inapata uangalizi mzuri.
‘’Gari ni ya kwetu tunapaswa kuitunza kwa hali na mali na hizi zote ni jitihada za viongozi wetu wa ngazi za juu wanaoisaidia serikali yetu kusikia kilio chetu cha sisi kutaka gari na kilio chetu na leo tumekabidhiwa gari ya Sh milioni 240.
’’Amesema Kapende.
Kapende ameishukuru serikali kwa jitihada iliyofanya kuwapatia kitendea kazi kitachosaidia kuwabebea wangojwa katika halmashauri hiyo.
Mganga Mkuu wa Halmashauri hiyo, Dickson Masale amesema awali halmashauri hiyo ilikuwa na gari moja tu la kubebea wagonjwa.