Nape ataka posta wawe wabunifu kujitangaza

WAZIRI  wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Nape Nnauye, ameliagiza Shirika la Posta Tanzania (POSTA) kuwa wabunifu katika kutangaza shughuli wanazozifanya, ili huduma zao ziweze kuleta tija kwa wananchi.

Waziri Nape amesema hayo wakati wa hafla ya uzinduzi wa Biashara ya Bima ya Shirika la Posta (Posta Insurance Broker) mjini  Arusha, leo Julai 28, 2023. 

“Kuanzishwa kwa huduma au biashara ni jambo moja, lakini kuwafikia walengwa ndiyo jambo la msingi, hivyo nawaelekeza Posta ili muweze kufikia malengo, nguvu kubwa inahitajika katika kuitangaza biashara yenu katika vyombo vya habari, na kuwafuata walengwa walipo kupitia njia mbalimbali ikiwemo mikutano na semina mbalimbali ili kuwapa elimu ya umuhimu wa bima hasa wale wakulima wa vijijini ambao ofisi nyingi za Posta ndiko ziliko,” amesema Waziri Nape na kujongeza:

“Kuna baadhi ya huduma nyingine za Posta zitazidi kufahamika kwa jamii kupitia wateja wapya watakaofika katika ofisi za Posta kupata huduma za Bima. Mteja anapofika kupata huduma hiyo atakutana na huduma nyingine zitakazomvutia zaidi, “ amesema Waziri Nape.

Katika hatua nyingine Waziri Nape amewapongeza Shirika la Posta kwa ubunifu waliofanya wa kuanzisha Bima hiyo kwani ni ishara tosha ya kuunga jitihada za Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Rais  Dk Samia Suluhu Hassan katika kuhakikisha kuwa Watanzania wengi wanapata fursa ya kuunganishwa na mifumo rasmi ya watoa huduma mbalimbali mahali pamoja, ili kurahisisha huduma kwa jamii, hivyo kuharakisha ukuaji wa uchumi wa wananchi na taifa hili kwa ujumla.

#TanzaniayaKidijiti #PotaKidijitali #PostaBima #KaziIendelee

Habari Zifananazo

Subscribe
Notify of
guest
3 Comments
Oldest
Newest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments
Nancy J. Serrano
Nancy J. Serrano
2 months ago

Working part-time, I bring home almost $13,000 per month. I was keen to find out after hearing several others describe how much money they were able to make online. Well, it all came to pass and completely altered my ba-07 life. Now, everyone needs to try this work by using this website.
.
.
Detail Are Here————————— https://fastinccome.blogspot.com/

Last edited 2 months ago by Nancy J. Serrano
yokiba9670
yokiba9670
Reply to  Nancy J. Serrano
2 months ago

Make money online from home extra cash more than 18000 to 21000 Dollars. Start getting paid every month Thousands Dollars online. I have received 26000 Dollars in this month by just working online from home in my part time. every person easily do this job by.
.
.
.
HERE====)>>> https://julizaah9.blogspot.com/

Last edited 2 months ago by yokiba9670
Money
Money
2 months ago

Taulo za kike

Tangazo.PNG
Back to top button
3
0
Would love your thoughts, please comment.x
()
x