Nape atoa ufafanuzi data za simu

WAZIRI wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Nape Nnauye (pichani) amebainisha kuwa serikali chini ya uongozi wa Rais Samia Suluhu Hassan imefanikiwa kupunguza bei ya data inayotozwa kwenye simu kutoka Sh 40.04 Machi, mwaka jana hadi Sh 9.35, mwezi huu.

Nape alitoa ufafanuzi kupitia ukurasa wake wa Twetter kutokana na baadhi ya watu kulalamikia bei kubwa ya data inayotozwa kwenye simu nchini. “Kwa heshima ya wale waliouliza maswali ya data kwa nia ya kuelewa na kujadiliana kwa staha kwa lengo la kupata muafaka, kwamba Rais Samia hajachukua hatua juu ya jambo hili, si kweli. Bei ya juu Machi, mwaka 2021 ilikuwa shilingi 40.04 na bei ya juu Agosti, mwaka 2022 ni shilingi 9.35,” aliandika.

Jedwali la bei za data kwa MB moja kwenye soko la rejareja kwa Machi mwaka jana, linaonesha wastani wa bei ya chini ya data ndani ya vifurushi ilikuwa Sh 1.11 na bei ya juu Sh 2.80. Lilionesha pia MB moja nje ya vifurushi ya chini ilikuwa Sh 24.16 wakati bei ya juu ilikuwa Sh 94.

“Kwa hiyo ukisoma majedwali haya mawili utaona kuwa kazi ya kwanza ya Serikali ya Awamu ya Sita ilikuwa kutoa bei ya juu ilikokuwa imefika yaani shilingi 40.4 kurudi mpaka shilingi 9.35, inawezekana kwa wengine hili si jambo kubwa lakini ni kweli si jambo kubwa?” alisema.

Alieleza kuwa kama ulivyo uzalishaji wa bidhaa nyingine zozote, zipo gharama za kuzalisha uniti moja inayosafirisha data. Alisema serikali inaendelea kuona namna gani itapunguza gharama za kuzalisha data nchini ili bei yake ishuke na kazi ya kwanza kufanikisha hilo, ilikuwa kupata uhalisia wa bei ya data.

“Halafu ndio unaangalia kitu gani kinaweza kufanywa ili kupunguza gharama za uzalishaji kusaidia kupunguza bei ya data. Ndiyo kazi serikali tunaendelea nayo tuone maeneo gani yakiguswa yatapunguza bei ya kuzalisha. Katika mazingira ambayo gharama za uzalishaji zinaongezeka,” alisema.

Nape alifafanua kuwa vifurushi ambavyo ni huduma ya ziada ambayo kwa Tanzania imegeuzwa kuwa huduma ya msingi Machi, mwaka jana, ilikuwa Sh 1.

11 mpaka Sh 2.80 na baada ya kutengeneza msawazisho wa kupunguza ya juu ndio wastani ukawa Sh 1.75 mpaka Sh 4.67.

Hata hivyo, katika ukurasa wake huo, ameendelea kuwataka Watanzania wenye malalamiko kuhusu bei zinazotozwa katika huduma za simu kuleta ushahidi kama zinatozwa zaidi hatua zichukuliwe.

Habari Zifananazo

Back to top button