Nape: Someni magazeti kwa ubunifu

Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Nape Nnauye

DAR ES SALAAM: Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Nape Nnauye, amesema kuwa ameruhusu waandishi wa habari kusoma magazeti kwa ubunifu.

Kupitia mtandao wake wa X zamani Twitter Nape ameandika “Nimeona mjadala wa “kusoma magazeti”.

“Nimeelekeza TCRA kuruhusu ubunifu  kwenye tasnia ya Habari. Staili ya usomaji we magazeti imeongeza mvuto kwenye usomaji huo, ni jambo linapaswa kutiwa moyo badala ya kuzuiwa. Waandishi endeleeni na ubunifu kwenye kusoma magazeti,”ameandika Nape

Advertisement

Kauli ya Nape imekuja baada ya jana,  Mhandisi Andrew Kisaka, Mkuu wa Kitengo cha leseni TCRA, kusema kuwa waandishi wa habari wanaoongeza mbwembwe kwenye usomaji wa magazeti na baadhi kuongeza  vitu visivyotakiwa wakati wa usomaji  watachukuliwa hatua.

Kisaka aliyasema hayo katika mkutano wa mwaka wa Vyombo vya Utangazaji Nchini uliofanyika Jijini Dodoma.

Alinukuliwa “Kuna wachache wakorofikorofi wanaleta mbwembwe na kuongezea vitu pale kwenye magazeti kwahiyo nafikiri hao pia watamulikwa na kushughulikiwa kwa mujibu wa kanuni na sheria, ni wachache sana”

Hata hivyo, leo Kisaka amenukuliwa akisema kuwa  kauli yake ilitafsiriwa vibaya alichopiga marufuku ni usomaji wa magazeti kusoma kwa kina habari nzima na badala yake wasome vichwa vya habari tu kama sheria inavyosema