Nape: Uhuru wa vyombo vya habari nchini umeimarika

DODOMA: Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Nape Nnauye, amesema hali ya uhuru wa vyombo vya habari nchini imeimarika ikilinganishwa na ilivyokuwa awali.

Waziri Nape ameyasema hayo leo Mei 03,2024 kwenye maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari Duniani yaliyofanyika kwenye ukumbi wa mikutano wa Jakaya Kikwete, jijini Dodoma na kusema hali hiyo inazidi kuimarika.

“Hali ya uhuru wa vyombo vya habari nchini inaendedelea kuimarika. Bado hatujafika tunakotaka kwenda lakini kwa hakika hatupo tulipokuwa jana. Tumefika hapa kutokana na juhudi za Mheshimiwa Rais, tumetekeleza 4R za Mheshimiwa Rais na ndiyo maana tuko hapa tulipo,” amesema.

Advertisement

Kaulimbiu ya maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari Duniani kwa mwaka 2024 ni “Uandishi wa Habari na Changamoto za Mabadiliko ya Tabianchi”.