Napoli bingwa ‘Serie A’
BAADA ya takribani miaka 33, klabu ya Napoli hatimaye imetwaa ubingwa wa Ligi Kuu nchini Italia maarufu kama ‘Serie A, kufuatia sare ya 1-1 dhidi ya Udinese Uwanja wa Dacia Arena, Udine.
–
Ubingwa huo ni watatu katika historia ya timu hiyo. Sherehe za shangwe miongoni mwa wachezaji na pia katika jiji la kusini mwa Italia, ambao wengi wao walikuwa wamekusanyika katika uwanja wa Stadio Diego Armando Maradona.
–
Kombora la Sandi Lovric liliwapa Udinese bao la kuongoza kipindi cha kwanza, lakini fowadi wa Napoli, Victor Osimhen akafanya matokeo kuwa 1-1 mapema katika kipindi cha pili.
–
Osimhen, ambaye ndiye mfungaji bora wa Serie A msimu huu, amekuwa ufunguo wa mafanikio ya Napoli na hili lilikuwa bao lake la 22 la ligi msimu huu.
–
Kombora la Sandi Lovric liliwapa Udinese bao la kuongoza kipindi cha kwanza, lakini fowadi wa Napoli, Victor Osimhen akafanya matokeo kuwa 1-1 mapema katika kipindi cha pili, akiongoza mpira nyumbani baada ya shuti la Khvicha Kvaratskhelia kuokolewa kufuatia kona.
–
Osimhen, ambaye ndiye mfungaji bora wa Serie A msimu huu, amekuwa ufunguo wa mafanikio ya Napoli na hili lilikuwa bao lake la 22 la ligi msimu huu.
–
Mnigeria huyo mwenye umri wa miaka 24 alifunga bao lake mbele ya mashabiki wa Napoli waliosafiri, ambao walishangilia bao la kusawazisha kwa mbwembwe zote.
–
Baada ya sare hiyo, Napoli amefikisha pointi 80 ambazo haziwezi kufikiwa na timu yoyote huku ikiwa imebaki michezo mitano kabla ya ligi kumalizika.