Nay wa Mitego Nay wa Mitego kuibukia A. Kusini

Emmanuel Elibariki ‘Nay wa Mitego’

RAPA wa muziki wa Hip hop nchini, Emmanuel Elibariki ‘Nay wa Mitego’ amesema ana mpango wa kwenda Afrika Kusini kufanya wimbo mpya na mmoja wa wasanii wakubwa nchini.

Akizungumza na HabariLEO, Rapa huyo alisema kuwa sababu kubwa ya kutaka kufanya hivyo ni kutaka kubadilisha ladha na kutanua wigo kwenye biashara zake za muziki.

“Nataka kujitambulisha kimataifa zaidi, nilishawahi kufanya kazi na wasanii wa nje lakini kitambo kidogo hivi sasa nimejipanga kuhakikisha lengo langu la kuunyanyua muziki wa Hip hop linatimia tena kwa mafanikio makubwa,” alisema Nay wa Mitego.

Advertisement

Msanii huyo alisema anawaheshimu wasanii waliopo nchini pamoja na kazi zao lakini yeye angependa kufika mbali zaidi hasa kutokana na ukomavu wake kwenye muziki huo ambao umempa umaarufu mkubwa nchini.