NBAA watumia michezo kusaidia wagonjwa wa saratani

BODI ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu Tanzania (NBAA), imeendesha michezo mbalimbali yenye nia ya kuchangisha fedha kusaidia watoto wanaougua magonjwa ya saratani katika Hospitali ya Taifa Muhimbili.

Michezo hiyo ni mbio za kilomita tano na 10, michezo ya kuogelea, ambayo ilihusisha washiriki wa kongamamo la Wahasibu leo jijini Dar es Salaam.

Advertisement

Akizungumza baada ya michezo hiyo, Mkurugenzi wa Huduma za Viwango vya Kiuhasibu, Utafiti na Huduma za Ufundi wa NBAA, Angyelile Tende, amesema lengo la kuendesha michezo hiyo ni kuhamasisha washiriki kuchangia fedha.

Amesema washiriki waliojitokeza katika michezo hiyo ni 800 na kwamba lengo lao limekamilika kama walivyopanga. Kongamano hilo la Bodi ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu Tanzania linatarajiwa kufungwa kesho.

2 comments

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *