NCC kukamilisha mwongozo gharama ujenzi barabara

BARAZA la Taifa la Ujenzi (NCC) lipo mbioni kukamilisha mwongozo wa gharama za msingi ( bei elekezi ) za ujenzi na ukarabati wa barabara nchini zitakazotumiwa na wakandarasi kila mkoa Tanzania Bara.

Mtendaji Mkuu wa NCC, Dk Matiko Mturi alisema hayo mjini Morogoro wakati wa kikao kazi cha kupitia viwango vya bei elekezi kwa ajili ya ujenzi wa barabara na ukarabati wa barabara kilichohusisha wataalamu wa taasisi za ujenzi, vyama vya wakandarasi , wakadiriaji majenzi na wahandisi washauri wa miradi.

Dk Mturi alisema ,hivi sasa kuna malalamiko mengi kwa baadhi ya wakandarasi kuweka bei ndogo na wanapopata miradi na wakienda katika utekelezaji wanapata kazi ngumu kuitekeleza hiyo miradi.

Mtendaji mkuu wa NCC alisema, kukamilika kwa miradi hiyo inawalazimu kuisimamia kwa karibu zaidi na pia kwa kuweka kiwango cha chini kunachangia kukosekana kwa ushindani.

“ Unapokuwa na mkandarasi moja anaweka bei halisi na mwingine anaweka bei ndogo hawatashindana na kwa utaratibu wetu ( serikali) mtu mwenye bei ya chini ndiye anapewa kazi na yule mwenye bei kubwa hatapewa “ alisema Dk Mturi

Dk Mturi alisema,uzoefu uliopo wenye kuweka bei ndogo wakienda eneo la mradi (Site) wanakabiliana na chagamoto nyingi ikiwemo ya kusababisha utekelezaji wa mradi unachukua muda mrefu na wakati mwingine hauridhishi.

“ Na sisi ambao tunatoka serikalini ina maana umsimamie huyu mtu kama vile wewe ndiye unatengeneza …hiyo ile tunataka tuiondoe “ alisema Dk Mturi

Dk Mturi alisema baada ya kumaliza kufanya maboresho ya mwongozo huo, baraza litatengeneza mfumo wa kielekroniki utakaowezesha mwongozo kupatikana kirahisi hata kwenye simu kwa kutumia mtandao wa intaneti .

Alisema mwongozo huo umegawanyika sehemu mbili , eneo moja ni la taarifa za gharama za vifaa vya ujenzi na nyingine ni mfumo wa ukokotoaji wa taarifa za gharama za ujenzi kutoka maeneo mbalimbali zilizoingizwa katika mfumo huo utakaokujulisha gharama halisi za vifaa eneo husika .

“ Hizi taarifa za gharama za ujenzi zinabadirika kila siku , tunacho kwenda kufanya ni kukusanya taarifa za bei ya sasa ili kila mara kutoa bei ambazo zinaakisi gharama za wakati huo “ alisema Dk Mturi

Dk Mturi alisema , Baraza litafanya majaribio ya mfumo huo kwenye baadhi ya miradi ili kuona unavyofanya kazi na kwamba maboresho yanafanyika yatakapohitajika.

Hivyo alisema baada ya kukamilika,Serikali itaweka rasmi mwongozo huyo kaatika mfumo wa ununuzi au utekelezaji wa gharama za ujenzi.

“ Baada ya kutathimini na kuona unafanya kazi vizuri hakutakuwa tena na kila mtu kuandaa gharama zake” alisema Dk Mturi

Dk Mturi alisema gharama hizo zinafanyiwa marejeo kila baada ya miezi mitatu ili kuzifanya kila wakati zinaakisi gharama za soko kwa wakati huo.

Alisema kuandaa mwongozo huo imekuwa ni kazi ya msingi na ilianza mwaka 2020 kwa wataalamu wa Baraza hilo kupita katika miradi ya barabara mbalimbali kuangalia utendaji kazi wa eneo husika na kazi moja moja inayotekelezwa.

Dk Mturi alisema miongoni mwa mambo yaliyoangaliwa ni rasilimali zinazotumika kwenye hiyo miradi hiyo na kusikiliza maoni yao kuhusu gharama zinazotumika kwa sasa katika utekelezaji wa miradi hiyo.

Alisema mwongozo huo unaandaliwa ili kuwezesha serikali inapohitaji kujenga miradi inakuwa na bajeti ya makisio kwa kiasi kikubwa yanatokana na gharama za ujenzi wa kilometa moja ya barabara ( Unit Cost).

“ Na hizo kilometa moja za Barabara inajengwa kwa kiasi gani inapatikana kwa kuwa na gharama za ujenzi au ukarabati wa kazi moja moja ambazo zinawezesha kujenga kila kilometa moja “ Unit Rates” alisema Dk Mturi

“ Tumekusanya taarifa za gharama za vifaa vya ujenzi kutoka katika kila mkoa wa Tanzania na pia kutoka katika sehemu maalumu kwenye kisiwa cha Mafya na Ukerewe “ alisema Dk Mturi

“ Nia yetu ni kuonesha ya kwamba ukijenga hapa barabara Morogoro na ukujenga sehemu nyingine sinatofautiana lakini pia tunatambua hizi barabara zinauwezo tofauti , barabara ambayo inabeba magari mengi na barabara inayobena magari machache ni tofauti” alisema Dk Mturi

Habari Zifananazo

Back to top button