NCCR Mageuzi waipa tano serikali mkataba na Dp World

CHAMA cha NCCR Mageuzi kimeipongeza serikali kuingia mkataba na DP World kuwa una manufaa zaidi kwa watanzania kwani serikali inapata asilimia 60 na DP World inapata asilimia 40

Akizungumza Makao Mkuu ya Chama hicho Ilala jijini Dar es Salaam, Makamu Mwenyekiti wa NCCR Mageuzi, Joseph Selasini amesema wao kama NCCR waliitikia wito wa Rais Samia Suluhu Hassan na kiungwana uwezi kugomea wito wa Rais wa nchi.

“Mwaliko umekuja sio jukumu letu kuhoji mualiko umekujaje au kwa nini nimealikwa, unachopaswa kufanya ni kuitikia mwaliko na kwenda kusikiliza na kuchambua yale unayoelezwa.”Amesema Selasini na kuongeza

“Utafanya maamuzi kulingana na ufahamu wako na vile unavyoweza kuelewa, uwezi kupewa mwaliko na Rais ukaukataa, ndio maana tuliudhuria na wengine waliudhuria, kuwe na ajenda kusiwe na ajenda au ajenda yenye mashaka, hoja ya kiungwana uwezi kukataa wito, kata maneno sio wito.”Amesisitiza

Amesema kuongoza ni kuvumilia, kiongozi mzuri lazima aonyeshe kiwango cha juu cha uvumilivu.

“Baada ya mkataba wa awali IGA kupitishwa bungeni watanzania na taasisi nyingi zikiwemo za dini walilalamika na kutoa maoni mbali mbali;…… ““Mkataba wa awali haufanani na mkataba kamili, IGA ni mkataba wa awali.”Amesema na kuongeza

“Tunataka serikali itengeneze timu ya kufaa ya wazalendo watakaofuatilia kwa maslahi ya Watanzania utekelezwaji wa mkataba wa DP World, kama mkataba wa DP World  utatekelezwa utakuwa na faida kubwa sana kwa Watanzania.”Amesema   Selasini

Amesema kuunga kwao  mkono swala la bandari ni maoni yao  na hawajalazimishwa na mtu yoyote kuunga mkono maoni yake, wala hashurutishwa kwa namna yeyote na wala hawaogopi juu ya hilo waliloamua.

“Haya ni maoni yetu hayausu chama chochote cha siasa wala dini, kama tunasema tunajenga Demokrasia hivyo maoni yetu yanaweza yasifanane na vyama 18 vya siasa vilivyosalia,  wala mtu yeyote kwa vile akili pia hazifanani.

“Chama chetu si chama cha kupinga pinga tu kila kitu, haiwezekani mambo kumi yafanyike kwasababu sisi ni wapinzani tuogope kuyasema mazuri yaliyofanywa, tupambane tu kwasababu sisi ni wapinzani hapana,”amesema

Amesema wamesikiliza hoja zote  ambazo watanzania walikuwa wanazilalamikia na kuzitolea mapendekezo zilipatiwa majibu, hoja ya kwanza kubwa kuliko zote ilikuwa ianzishwe kampuni ya watanzania ambayo itaingia ubia na DP World ambapo mkataba uliopo sasa Tanzania inapata asilimia 60 na DP World asilimia 40

“Sasa ni jambo tulilopigia kelele,  serikali imetuambia jambo hili imelichukua sisi sote sio watendaji wa serikali hatuwezi kuingia katika chungu kusema tuone, tukifikia huko maana yake ni kwamba hatuamini Baraza la Mawaziri, hatuamini makatibu wakuu na hatuamini mtu yeyote…..; “Tusipoaminiana nchi itakuwa inakwenda namna gani.”Amesema

Aidha, amesema jambo la pili ilikuwa ni ukomo wa mkataba, ambapo awali ilisemekana  mkataba ni wa milele kwa vile haukua na uwazi.

“Iila huu mpya uliongiwa unasema mkataba utakuwa wa miaka 30 lakini kila baada ya miaka mitano inaweza ukarejewa ama na DP world au serikali kulingana na mkataba utakavyokua.” Amesema

Kauli ya Selasini imekuja ikiwa ni siku 10 zimepita tangu serikali iingie mikataba mitatu na DP World Oktoba 22, Chamwino mjini Dodoma ambayo ni mikataba ya nchi mwenyeji (HGA), mkataba wa ukodishaji na uendeshaji wa gati 4 – 7, na uendeshaji wa pamoja wa gati 0 – 3 kati ya TPA na DP World kwa shughuli za kibiashara na za kiserikali.

 

 

 

 

Habari Zifananazo

3 Comments
Oldest
Newest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments
Back to top button