Nchi sita kushiriki gofu Arusha

WACHEZAJI zaidi ya 100 kutoka nchi zaidi ya sita wanatarajiwa kushiriki mashindano Ya “Inspire African Golf Open” yatakayofanyika Katika Uwanja wa Kili Jijini Arusha.

Akizungumza na waandishi wa habari katibu wa mashindano kutoka Chama Cha Golf Tanzania (TGU) Injinia Enock Magile amezitaja baadhi ya nchi kuwa Ni Tanzania, Kenya, Uganda, Ghana, Afrika Kusini Kongo, na Nigeria huku zoezi la kujiandikisha likiendelea.

Amesema Maandalizi ya Mashindano hayo yamekamilika na yanatarajiwa kuchukua siku tatu Kwa kuanza na wachezaji wa Kulipwa.

Kwaupande wake Mwenyekiti wa Festac ambao ndio waaandaji wa shindano hilo Yinka Abioye amesema Shindano Hilo lenye Lengo La kudumisha umoja wa nchi za Kiafrika Pamoja na Tamaduni zake Huku zawadi za kipekee zitatolewa kwa washindi siku hiyo .

Shindano hilo la “Inspire African Golf Open” litaanza Ijumaa kwa Wachezaji wa kulipwa na Jumamosi na Jumapili Kwa Wachezaji wa Ridhaa wakiweno wanawake na watoto.

Habari Zifananazo

1 Comment
Oldest
Newest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments
Back to top button