Nchimbi: Waambieni wananchi maendeleo

KATAVI: Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi Dk Emmanuel Nchimbi amewataka viongozi mbalimbali nchini kuwa na utaratibu wa kuwataarifu wananchi juu ya kazi za maendeleo zinazofanywa na Serikali ili kupunguza maswali kwa wananchi.
Ameyasema hayo akiwa katika ziara yake ya kwanza mkoani Katavi alipokuwa akitoa salam za Chama katika ofisi ya CCM mkoa ambapo kabla ya yote ametoa tahadhari ya kutosikiliza kero ambazo zinaendelea mahakamani.
Dk Nchimbi tayari ameanza ziara yake mkoani Katavi kati ya mikoa sita atakayotembelea ya ambayo ni Katavi,Rukwa,Songwe,Mbeya, Njombe na Ruvuma.

Habari Zifananazo

Back to top button