Ndalichako ataka mifumo ufanyaji mazoezi

WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Joyce Ndalichako amewataka waajiri nchini kuweka mifumo endelevu itakayohakikisha wafanayakazi wanapata fursa ya kuimarisha afya kuelekea maadhimisho ya ugonjwa wa afya akili duniani.

Ndalichako ametoa wito huo leo Oktoba 7, 2023 katika bonanza la waajiri iliyowakutanisha waajiriwa kutoka sekta mbalimbali ambayo imeandaliwa na Chama cha Waajiri Tanzania (ATE) lengo ni kuendelea kuimarisha afya zao na kufanya kazi kwa ufanisi na kuongeza uzalishaji.

Advertisement

Amesema kumekuwa na matukio mbalimbali yanayotokana na wengi wao kuwa na msongo wa mawazo katika maeneo ya kazi na kupelekea kupoteza maisha na hivyo waajiri wachukue hatua za makusudi kupunguza shida hiyo.

Aidha, amesema serikali itaendelea kuboresha mazingira ya kazi na kuweka mifumo thabiti ya kuhakikisha kuwa nguvukazi ya taifa.

Katibu Mkuu wa Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi (TUCTA) Hery Mkunda akizungumza kwa niaba ya wafanyakazi wote nchini amesema wataendelea kushirikiana na ofisi ya Waziri Mkuu kuhakikisha kila mfanyakazi anakuwa na mazingira bora ya utendaji.

Awali akifanya utambulisho, Mtendaji Mkuu wa ATE,  Suzanne Ndomba amesema bonanza hiyo imelenga kuimarisha afya ya kwa wafanyakazi wa Ili watende kazi Kwa ufanisi na kupunguza migogoro isiyokuwa ya lazima.

Mtendaji Mkuu wa usalama na afya mahala pakazi, Khadija Mwenda amesema jukumu kubwa walilonalo ni kuhakikisha sehemu zote za kazi zinakuwa salama na  kwamba wataendelea kuwashauri wa wafanyakazi kuweka utaratibu kuangalia afya zao marakwa mara.

Bonanza hiyo imefanyika ikiwa ni kuelekea Kilele cha Maadhimisho ya Afya ya Akili Duniani yatakayofnyika Oktoba 10 mwaka huu na kauli mbiu ya ni kuimarisha afya ya akili ili kuongeza tija mahali pa kazi.

3 comments

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *