Ndalichako: serikali itaendelea kushikamana na sekta binafsi

DAR ES SALAAM: WAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu. Prof, Joyce Ndalichako amesema serikali itaendelea kuthamini mchango na kazi zinazofanywa na sekta binafsi katika kutatua changamoto ya ukosefu wa ajira hapa nchini.

Ametoa kauli hiyo jijini Dar es salaaam wakati akimwakilisha Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa kwenye ugawaji wa tuzo za  mwajiri bora wa mwaka 2023 zilizoandaliwa na chama cha waajiri Tanzania (ATE).

Ndalichako amesema kuwa waajiri wazingatie sheria ya watu wenye ulemavu inayowataka kuwaajiri  asilimia 3% kati ya watu 20 iwe ya wenye ulemavu .

Advertisement

Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa chama cha waajiri Tanzania (ATE), Suzanne Ndomba amesema  tangu kuundwa kwa tuzo hizo za mwajiri bora wa mwaka zimekuwa zikihamasisha makampuni kuweka juhudi katika maswala ya usimamizi wa rasilimali watu kwa kufata sheria , kuweka sera, kanuni na mazingira bora ili kuongeza tija kwa waajiri.

Kwa upande wake Mkurugenzi mkuu wa Mamlaka ya usafiri wa anga (TCAA), Hamza Johari  akizungumza baada ya kutwaa tuzo ya pili katika kipengele cha mwajiri bora sekta ya Umma amesema tuzo hiyo ni chachu kwa taasisi yao kwani italeta chachu ya kufanya vizuri zaidi kwa taasisi hiyo.

Katika tuzo za mwaka huu ambazo taasisi na makampuni 1500 yalionesha nia ya kushiriki ni taasisi 91 pekee zilizokidhi viwango kwenye tuzo hizo.

 

1 comments

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *