Ndayishimiye: Jumuiya ya Kimataifa isaidie DRC

RAIS Evariste Ndayishimiye ameahidi kwamba nchi yake itaisaidia Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) kupambana na makundi ya waasi katika eneo la Mashariki kwa kutuma wanajeshi wake kufanya kazi hiyo.

Kiongozi huyo ambaye wanajeshi wake tayari waliingia Mashariki mwa DRC kupambana na waasi wa Red Tabara na kuchangia katika Kikosi cha Jeshi la Jumuiya ya Afrika Mashariki ili kuleta amani Mashariki mwa DRC, ameiomba jumuiya ya kimataifa kuisaidia DRC kuondokana na tatizo hilo.

“Burundi haitachoka kuchangia wanajeshi wake kwa ajili ya amani katika nchi zenye vita. Tutafanya hivyo kwa kuzingatia kanuni za Umoja wa Mataifa, Umoja wa Afrika na mikataba mingine,” alisema Ndayishimiye.

Akaongeza: “Kwa sasa wanajeshi wetu wanalinda amani nchini Somalia na Afrika ya Kati. Burundi imejitolea kusaidia kurejesha amani huko DRC chini ya makubaliano ya Jumuiya ya Afrika Mashariki.”

“Nachukua fursa hii kuomba jumuiya ya kimataifa kuunga mkono makubaliano ya Nairobi, kuisaidia DRC.”

 

 

 

 

 

 

Habari Zifananazo

Back to top button