WATU watano wamekufa na wengine wawili kujeruhiwa kufuatia ndege moja iliyokuwa imebeba watu saba kuanguka baada ya kushindwa kuruka Mashariki mwa Burkina Faso, mamlaka ilisema.
Ndege hiyo ilikuwa ikipaa kutoka katika uwanja wa ndege wa eneo hilo katika jiji la Diapaga ikielekea mji wa Fada N’Gourma ikaishi kuangukia kwenye mti, shirika la habari la serikali la Agence d’Information du Burkina lilisema.
Watu wawili waliojeruhiwa walikimbizwa katika kituo cha afya, na mamlaka ilikuwa imeanza uchunguzi kuhusu ajali hiyo, Wizara ya Usafiri ya Burkina Faso ilisema katika taarifa.
Haikuweza kufahamika mara moja kwa nini ndege hiyo haikuweza kupaa kwa mafanikio.