Ndejembi ataka uzalendo kwa maofisa uchunguzi TAKUKURU

NAIBU Waziri Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Deo Ndejembi amefunga mafunzo ya awali ya miezi mitano kwa maafisa uchunguzi na maafisa uchunguzi wasaidizi wa TAKUKURU 536.

Akizungumza wakati wa kufunga mafunzo hayo katika Chuo Cha Polisi CCP Moshi, Naibu Waziri Ndejembi amewataka maafisa hao kwenda kufanya kazi kwa weledi, uadilifu na kutanguliza uzalendo mbele ili kulinda imani ya wananchi kwa Serikali yao.

“Niwasihi nyote ambao mmehitimu mafunzo haya kwenda kufanya kazi kwa uadilifu, Serikali chini ya Rais Samia imewekeza fedha nyingi katika kutekeleza miradi ya maendeleo hivyo ni jukumu lenu kama maafisa uchunguzi kuhakikisha hakuna fedha yeyote ya Serikali inapotea kwenye miradi hiyo,” ameeleza na kuongeza:

Naibu Waziri Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma Deo Ndejembi

“Serikali imewaamini mafunzo haya yamegharimu takribani Sh bilioni mbili…Hatutegemei kuona baada ya kuanza kazi na kupangiwa vituo vyenu vya kazi mnaanza kuomba uhamisho, niagize hapa hakuna afisa yeyote ambaye atahamishwa kwenye kituo alichopangiwa kazi hadi baada ya miaka mitano,” Naibu Waziri Ndejembi.

Habari Zifananazo

Back to top button