Ndejembi, Mahundi wahamishwa wizara

ZANZIBAR: RAIS Samia Suluhu Hassan amemteua Degratious Ndejembi kuwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, (Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulevamu).

Kabla ya uteuzi huo, Ndejembi alikuwa Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais- Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI)

Taarifa iliyotolewa muda huu na Mkurugenzi wa Mawasiliano Ikulu, Zuhura Yunus imeeleza kuwa Rais Samia amemteua Zainabu Katimba kuwa Naibu Waziri wa Tamisemi.

Taarifa hiyo imeeleza kuwa Daniel Sillo ameteuliwa kuwa Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, akichukuwa nafasi ya Jumanne Sagini ambaye amehamishwa kuwa Naibu Waziri Katiba na Sheria.

Aidha amemhamisha Maryprisca Mahundi kutoka Wizara ya Maji na kuwa Naibu Waziri wa Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari.

Pia Rais Samia amemhamisha Kundo Mathew kutoka Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari kwenda kuwa Naibu Waziri wa Maji.

Habari Zifananazo

Back to top button